Dhima ya mradi ilikuwa ni kuongeza ujuzi kuhusu namna ya kutekeleza huduma za matibabu maalumu, hasa mifupa na kisukari pamoja na ujuzi wa vitendo kwa matabibu na watumishi wasaidizi wa Hospitali ya Mtakatifu Walburga: ambapo ilitarajjwa kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na taasisi hii. Dhumuni la mafunzo kwa matabibu na watumishi wasaidizi yaliyotolewa na watu wamaojitolea kutoka Poland ilikuwa kuwasilisha mbinu za matibabu ya kisasa, dalili za magonjwa na madhara ya tiba kama sehemu ya tiba kwa jinsi inavyofanyika Poland na Duniani kote. Mafunzo pia yanajumuisha kanuni za jumla katika tiba, mashauriano na taratibu za tiba. Mafunzo yaligawanywa katika sehemu ya nadharia na vitendo. Mradi pia ulihusisha shughuli zilizolenga kupanua ujuzi kuhusu magonjwa na matatizo yanatokea katika nchi zinazoendelea, wazo la kujitolea na malengo ya ushirikiano wa maendeleo wa kipolishi. Mradi ulichangia utekelezaji wa Lengo la tatu (3) la maendeleo endelevu, yaani kuhakikisha hali bora ya maisha kwa wote na afya njema kwa kila mmoja, bila kujali umri wao. Kwa matokeo ya Mradi huu kupitia mafunzo na mikutano iliyofanywa na watu wanaojitolea kwa matabibu na wahudumu wa afya wasaidizi wa hospitali ya Mtakatifu Walburga — Nyangao imewajenga ujuzi katika Nyanja za tiba za kisasa za magonjwa ya mifupa na kisukari. Pia zishukuriwe semina na mafunzo kwa vitendo kuhusu kipimo cha utendajikazi wa moyo (Electrocardio-ghaph): watumishi wa hospitali walipata uwezo wa kutumia kifaa bunifu kupelekea uboreshaji wa huduma za kila siku. Maarifa nadharia yalitolewa kupitia mikutano ya kila wiki kubadilishana uzoefu na kujadili hali za wagonjwa. Wafanyakazi wa hospitali walipokea vitu vya kujifunzia kwa njia ya ki-elektroniki na nakala za kuchapa zilizoandaliwa na watu wanaokitolea. Pia walitoa mapendekezo ya matibabu kwa wahudumu wa afya. Matokeo ya shughuli za kujitolea imechangia kiongezeka kwa Ubora wa hduma za matibabu zitolewazo kwa wagonjwa katika hospitali ya Mtakatifu Walburga Nyangao. Shughuli za hospitali zilipanuliwa kuhusisha huduma za wagonjwa wa kisukari kama sehemu ya kliniki ya wagonjwa nje ilianzishwa wakati huo. Nyanja ya dawa pia ilipanuliwa. Hali ya afya kwa kundi la wagonjwa wanaohudumiwa Nyangao hospitali imeboreshwa. Shukrani kwa mashauriano mfululizo na taratibu za matibabu yaliyotolewa na watu wanaojitolea, pamoja na utekelezaji wa kanuni za matibabu ya wagonjwa kufanikiwa kwa huduma zitolewazo Nyangao Hospitali na kuanzishwa kwa kipimo cha utambuzi wa magonjwa ya moyo (ECG) baada ya mafunzo kwa watumishi wote wa tiba. Mradi ulifanyika kati ya mwezi June 14 (kumi na nne) hadi Desemba 31 (thelathini na moja), 2016 (elfu mbili kumi na sita), ili kuendeleza taasisi na Dayosisi ya Kanisa Katholiki Lindi. Watu wanaojitolea walikuwa Nyangao mara mbili, mmoja alikuwepo kuanzia tarche mbili septemba elfumbili kumi na sita (2 Sept. 2016) hadi tarehe 13 oktoba, 2016; na wa pili kuanzia septemba 28, 2016 hadi Novemba 23, 2016.