Home » Bez kategorii » Ukarabati wa Maabara ya Vidusia/Parasitolojia katika LITA-Kampasi ya Tengeru(Arusha).

Ukarabati wa Maabara ya Vidusia/Parasitolojia katika LITA-Kampasi ya Tengeru(Arusha).

Kulingana na mradi wa “Uboreshaji wa ubora mafunzo ya afya ya Mifugo kwa vijana nchini Tanzania kwa kuboresha Mazingira na Mbinu za Kufundishia” Taasisi ya ‘Foundation Science for Development’ ya nchini Poland imeshaanza na inaendelea na ukarabati wa maabara ya vidusia katika wakala wa vyuo vya mafunzo ya mifugo,Kampasi ya Tengeru(Arusha). Baada ya ukarabati kukamilika maabara hii itatumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kuhusu vidusia/parasitolojia ya mifugo kwa wakufunzi na wanafunzi. Malengo ya awali ya ukarabati yaliongezeka mara tu baada ya wawakilishi wa taasisi hii kutembelea Kampasi na kujionea hali halisi. Kimsingi, ilionekana ni vyema ukarabati ujumuishe maboresho ya paa kwa kuondoa vigae chakavu vilivyodumu kwa zaidi ya miaka sitini na kuweka bati mpya na bora ili kutatua tatizo la paa kuvuja na kuwa kero hasa wakati wa msimu wa mvua. Uongozi wa Wakala uliahidi kulipa gharama zote za ufundi katika shughuli nzima ya ukarabati wa paa na mahitaji mengine muhimu kama mbao na Taasisi hii ya Kipolishi iliahidi kununua mabati kwa kutumia fedha za mradi. Mpango huu wa ukarabati umezingatia ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika Kampasi ya Tengeru na hivyo kupelekea upungufu wa vyumba vya maabara na vifaa vya kufundishia. Ili kukabiliana na changamoto hii Taasisi hii ilikubaliana na menejimenti ya Wakala wa vyuo vya mafunzo ya mifugo kufanya upanuzi wa maabara hii ya vidusia kwa kuvunja baadhi ya kuta ili kuongeza ukubwa wa chumba. Mradi huu unafadhiliwa kwa ushirikiano wa Foundation Science for Development na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kipolishi chini ya Programu ya Misaada ya Kipolishi.