TUZO YA “AMICUS OECONOMIE” KWA BWANA KRZYSZTOF BUZALSKI – BALOZI WA JAMHURI YA POLAND NCHINI TANZANIA.
Tulifurahi, kuhudhuria mkutano wa mwaka uliofanyika kabla ya Krismasi ambao ulihusisha muhtasari wa jumla wa masuala ya diplomasia ya uchumi yanayotambuliwa na Idara ya Ushirikiano wa Uchumi (MFA) na diplomasia ya Jamhuri ya Poland kwa kushirikiana na wawakilishi wa Poland katika maswala ya biashara, utawala/serikali, sekta binafsi, pamoja na mashirika na taasisi zinazofanya kazi katika kukuza uchumi wa Poland. Mkutano huo ulifanyika mnamo tarehe 10 Desemba, 2019. Pamoja na mambo mengine, hii ilikuwa ni fursa ya pekee ya kumkabidhi Bw Krzysztof Buzalski – Balozi wa Jamhuri ya Poland nchini Tanzania tuzo ya”The Amicus Oeconomiae“. Alikabidhiwa tuzo hii akiwa kama msimamizi wa chombo, ambacho hushiriki kikamilifu katika kukuza na kuunga mkono uchumi wa Kipolishi nje ya nchi. Tunampongeza sana Mheshimiwa Balozi na wafanyakazi wote wa Ubalozi jijini Dar-es-salaam, Tanzania.