Home » Bez kategorii » MRADI WA UBORESHAJI WA UBORA MAFUNZO YA AFYA/TIBA YA MIFUGO KWA VIJANA NCHINI TANZANIA KWA KUBORESHA MAZINGIRA NA MBINU ZA KUFUNDISHIA.

MRADI WA UBORESHAJI WA UBORA MAFUNZO YA AFYA/TIBA YA MIFUGO KWA VIJANA NCHINI TANZANIA KWA KUBORESHA MAZINGIRA NA MBINU ZA KUFUNDISHIA.

Taasisi ya Kipolishi ya Sayansi ya Msingi kwa Maendeleo (Foundation Science for Development) imekamilisha shughuli za mradi wake ujulikanao kama:“Uboreshaji wa ubora mafunzo ya afya/tiba ya Mifugo kwa vijana nchini Tanzania kwa kuboresha Mazingira na Mbinu za Kufundishia”zilizopangwa kwa mwaka wa 2019. Mradi huu unafadhiliwa kwa ushirikiano wa taasisi hii pamoja na Wizara ya Mambo ya Nchi za nje ya Kipolishi kwa mujibu wa programu ya misaada ya Kipolishi. Wanufaika wa mradi huu ni taasisi mbili zinazohusika na kutoa elimu/mafunzo katika eneo la afya/tiba ya mifugo nchini Tanzania ambazo ni: Chuo kikuu kishiriki cha Tiba ya Mifugo na Sayansi za afya ya viumbe cha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Morogoro (SUA), na Wakala wa Vyuo vya Mafunzo Mafunzo ya Mifugo (LITA) –Kampasi ya Tengeru (Arusha). Kwa mujibu wa utekelezaji wa malengo ya mradi huu vyumba viwili vya maabara vilikarabatiwa kwa ajili ya kuendesha shughuli za mafunzo. Aidha,baada ya shughuli za ukarabati kukamilika, vyumba hivyo vilifungwa vifaa vya kisasa vya maabara. Baada ya kazi ya ukarabati wa miundombinu muhimu kukamilika mafunzo maalumu yalifanyika kwa baadhi Wahadhiri na Wakufunzi wa taasisi za SUA na LITA. Mafunzo haya yaliendeshwa na Wahadhiri wa Kipolishi kutoka Chuo Kikuu cha Warsaw cha sayansi za uhai (Warsaw University of Life Sciences-SGGW) kitivo cha tiba/afya ya mifugo. Kupitia mafunzo haya wafanyakazi wa SUA na LITA walipata fursa ya kupanua ujuzi wao na maarifa ya msingi katika maeneo ya anatomia ya wanyama/mifugo na masuala ya kiliniki ya utambuzi wa magonjwa ya mifugo/wanyama. Shughuli za mradi huu zilizoanza mnamo mwaka 2019 zitaendelea tena kwa mwaka huu wa 2020.