Uboreshaji wa ubora mafunzo ya afya/tiba ya Mifugo kwa vijana nchini Tanzania kwa kuboresha mbinu na Mazingira ya Kufundishia.
Mradi na. 137/2019/M “Uboreshaji wa ubora mafunzo ya afya/tiba ya Mifugo kwa vijana nchini Tanzania kwa kuboresha mbinu na Mazingira ya Kufundishia”. Huu ni mradi mpya unaoendeshwa na taasisi ya Kipolishi ya Sayansi ya Msingi kwa Maendeleo (Foundation Science for Development). Mradi huu unawezeshwa na baadhi ya wahadhiri wa Kipolishi kutoka Chuo Kikuu cha Warsaw cha sayansi za uhai (Warsaw University of Life Sciences-SGGW) kitivo cha tiba/afya ya mifugo. Aidha, mradi huu ni sehemu ya Programu ya Misada ya Kipolishi (Polish Aid Program) na unafadhiliwa pia na Program ya Shirika la maendeleo la Kipolishi (Polands’ Development Coopration Program) chini ya Wizara ya mambo ya nje ya Jamhuri ya Poland. Wanufaika wa mradi huu ni: 1.Chuo kikuu kishiriki cha Tiba ya Mifugo na Sayansi za afya ya viumbe cha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-Chuo kikuu pekee cha Kilimo nchini Tanzania na; 2. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) –Kampasi ya Tengeru (Arusha) –Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Mifugo na uvuvi ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa utekelezaji wa malengo ya mradi huu vyumba vya maabara katika taasisi zote mbili vitaboreshwa na kuwa vya kisasa ikiwa ni pamoja na kuwekwa/kufungwa vifaa vya kisasa vya maabara. Aidha, kutakuwa na utaratibu maalum wa mafunzo kwa wakufunzi/wahadhiri na wataalam wa maabara ili kuboresha maarifa na uelewa wao katika fani ya utambuzi wa kimaabara wa magonjwa ya wanyama.